Mikopo
Utoaji wa mikopo kwa wanachama
Elimu SACCOS itatoa mikopo kwa wanachama wote wenye sifa ya kupata mikopo kwa kuzingatia upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kukopesha na kwa kuzingatia sera ya mikopo ya chama bila kuathiri sheria ya Huduma ndogo za fedha na Kanuni za huduma ndogo za fedha zinazosimamia SACCOS za mwaka 2019.
Sifa za mwanachama anayestahili kupata mkopo
Ili kuweka mazingira mazuri ya kuhakikisha mikopo inatolewa, baadhi ya mambo yafuatayo yatazingatiwa kabla mwanachama hajapatiwa mkopo ambapo mwanachama lazima awe na sifa zifuatazo;
- Awe mwanachama hai wa Elimu SACCOS alietimiza hisa za msingi na anaechangia akiba kila mwezi kama inavyoelekezwa kwenye Masharti ya Chama.
- Awe ametimiza miezi mitatu chamani tangu kujiunga kabla ya kuomba huduma ya mkopo chamani. ( Hii itategemea na uwezo wa chama kumhudumia mwanchama husika)
- Asiwe na mkopo alioshindwa kulipa wakati wa kuomba mkopo mwingine.
- Asiwe na mkopo alioshindwa kulipa kutoka taasisi nyingine.
- Awe na historia nzuri chamani katika urejeshaji wa mikopo yake
- Awe mshiriki mzuri kwenye shughuli za chama
- Awe na mradi unaotengeneza faida
- Awe na wadhamini wawili wenye akiba na hisa toshelezi kudhamini mkopo anaoomba.
Kwa maelezo zaidi kuhusu aina ya mikopo itolewayo na Elimu SACCOS pia utaratibu wa uombaji wa mkopo, sheria na taratibu mbalimbali pekua SERA YA MIKOPO YA ELIMU SACCOS ujue mengi zaidi.